Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | China yajiandaa kurusha chombo cha kuchunguza mwezi cha Chang'e-7
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 20, 2026
WENCHANG - Chombo cha kuchunguza mwezi cha Chang'e-7 cha China kimepangwa kurushwa kwa wakati unaofaa, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema katika taarifa ya jana Jumatano.
Jukumu la Chang'e-7 linalenga kufikia mafanikio mapya katika teknolojia mbalimbali muhimu, kama vile kutua kwa usahihi wa hali ya juu kwenye uso wa mwezi, mwendo kwa kutumia miguu, miruko ya kuchunguza kreta zenye kivuli cha kudumu.
Kwa mujibu wa CMSA, jukumu hilo litatumia mbinu kamili ya ugunduzi, ambayo inahusisha kuzunguka kwenye obiti, kutua, kuzunguka na miruko ili kufanya utafiti wa mazingira na rasilimali katika ncha ya kusini ya mwezi. Pia litahusisha ushirikiano wa kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




