Lugha Nyingine
Shughuli za Utalii wa vijijini zastawi katika Wilaya ya Wuyuan, Mashariki mwa China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2026
![]() |
| Watalii wakifurahia chai kwenye nyumba ya kuwapokea watalii katika Wilaya ya Wuyuan mkoani Jiangxi, mashariki mwa China, Agosti 26, 2026. (Xinhua/Hu Chenhuan) |
Wilaya ya Wuyuan katika Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China inajulikana kwa mandhari ya kupendeza ya vijiji vyake pamoja na vijiji vya kijadi vinavyohifadhiwa vizuri.
Katika wilaya hiyo kuna sehemu mbili zenye vivutio vya utalii vya daraja la 5A la kitaifa, na sehemu 12 zenye vivutio vya utalii vya daraja la 4A la kitaifa. Wilaya hiyo imekuwa ikihimiza shughuli za utalii wa vijijini na kuleta nafasi zaidi za ajira kwa wakazi wa huko kwa kupitia shughuli za utalii na ujasiriamali husika.
Leo hii, wilaya hiyo ya Wuyuan imekuwa na nyumba za kuwapokea watalii vijijini zaidi ya 1,300, na shughuli za utalii vijijini zinachangia moja kwa moja utoaji wa nafasi za ajira zaidi ya 80,000.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




