Wakazi na watalii wote walioathiriwa wahamishwa baada ya maporomoko ya udongo na mawe kutokea Xizang, China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2026
Wakazi na watalii wote walioathiriwa wahamishwa baada ya maporomoko ya udongo na mawe kutokea Xizang, China
Mkazi aliyehamishwa kutoka Kijiji cha Labi akiwa amepewa makazi mapya ya muda kwenye hosteli katika Kijiji cha Jifu cha Wilaya ya Gyirong, huko Xigaze, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Agosti 27, 2026. (Xinhua/Jigme Dorje)

GYIRONG, Xizang – Serikali ya mitaa ya huko imesema jana Alhamisi kuwa, wakazi walioathiriwa na maporomoko ya udongo na mawe yaliyotokea katika Wilaya ya Gyirong ya Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, wamepewa makazi mapya, na watalii wote waliokuwa wamekwama wamehamishwa. 

Serikali hiyo ya mitaa imesema kwamba wanakijiji na wafanyakazi wa ujenzi jumla ya 499 wote wamepewa malazi ipasavyo. Wakati huo huo, watalii 555 walioathirika wamehamishwa na kusafirishwa chini ya uratibu wa idara za utamaduni na utalii. Hivi sasa hakuna watalii waliobaki wakiwa wamekwama.

Idara za usafiri wa ndege za abiria pia zimejiunga na juhudi hizo za uokoaji na utoaji msaada. Hadi kufikia saa 9 alasiri jana Alhamisi, ndege za usafiri wa abiria zilikuwa zimesafirisha wafanyakazi 324 wa uokoaji na utoaji msaada na kupeleka tani 24 za zana na vifaa vya uokoaji, mahitaji ya kila siku na dawa na vifaa vya matibabu kwa eneo lililokumbwa na maafa, na kutoa uungaji mkono kwa ajili ya kukabiliana na dharura na kuhamisha wakazi walioathiriwa.

Maporomoko hayo ya udongo na mawe yalikumba Bandari ya Gyirong katika Wilaya ya Gyirong ya Xizang, juzi Jumatano asubuhi. Hadi kufikia saa 2 asubuhi jana Alhamisi, watu watatu wamefariki dunia, wengine 558 walikuwa bado hawajulikani walipo, wakati wanakijiji wawili wa huko wamekolewa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha