Lugha Nyingine
Uwezo wa kuzalisha umeme kwa jua wa China wazidi uwezo wa kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe kwa mara ya kwanza (2)
![]() |
| Picha hii iliyopigwa Juni 1, 2026 ikionyesha mradi wa kuzalisha umeme kwa jua katika Mji mdogo wa Sanxing wa Wilaya ya Shizhu, Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Huang Wei) |
BEIJING - Uwezo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua (PV) uliowekwa wa China umezidi uwezo wa kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe kwa mara ya kwanza, hali ambayo imefanya nishati ya jua kuwa chanzo kikubwa zaidi cha umeme cha nchi hiyo kwa uwezo uliowekwa, Mamlaka ya Kitaifa ya Nishati ya China imesema jana Jumanne.
Uwezo wa umeme wa nishati ya jua uliowekwa wa China ulifikia kilowati bilioni 1.286 mwishoni mwa Julai, ukizidi uwezo wa umeme wa makaa ya mawe wa kilowati bilioni 1.285, kwa mujibu wa mamlaka hiyo.
"Hii inaashiria hatua muhimu katika mpito wa China wa nishati ya kijani na kaboni chache," amesema Liu Zhiqiang, mtaalamu kutoka Baraza la Umeme la China, akiongeza kuwa mfumo mpya wa umeme wa nchi hiyo, ukiwa na nishati mpya kama msingi, unaanza kuwa halisi kwa mwenendo wa kasi.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, hadi mwishoni mwa Julai, nguvu ya nishati ya jua ilikuwa ikichukua asilimia zaidi ya 30 ya jumla ya uwezo wa uzalishaji wa umeme uliowekwa wa China. Imesema kuwa, kwa kupimwa kwa uwezo mpya ulioongezwa, sehemu hiyo iliongezeka kwa hadi asilimia zaidi ya 40 katika miezi saba ya kwanza ya 2026, ikisisitiza upanuzi wa haraka wa sekta hiyo ya nishati ya jua.
Mamlaka hiyo ya Kitaifa ya Nishati ya China imesema kuwa China imejenga mnyororo kamili wa sekta ya nishati ya jua unaohusisha utafiti na maendeleo, usanifu na utengenezaji jumuishi. Imesema maendeleo ya kiteknolojia, ikiwemo mafanikio mapya ya mara kwa mara katika ufanisi wa ubadilishaji wa nishati ya jua, yamesaidia kuchochea maboresho yasiyokoma na upunguzaji kwa haraka wa gharama.
Imesema maendeleo hayo ya kasi ya China ya nguvu ya nishati ya jua na aina nyingine za nishati mpya pia yanatoa mchango chanya duniani.
Kwa kuwa mfumo mkubwa na unaokua kwa kasi zaidi wa nishati mbadala duniani, mamlaka hiyo imesema China kwa sasa inasambaza asilimia zaidi ya 80 ya moduli za nishati ya jua na asilimia 70 ya vifaa vya nishati ya upepo kote duniani, hali ambayo imesaidia mpito wa kijani katika nchi nyingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




