Lugha Nyingine
Xi asisitiza juhudi endelevu za kuimarisha sekta ya utengenezaji wa hali ya juu viwandani
(CRI Online) Septemba 18, 2026
Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuendeleza juhudi za kupanua na kuimarisha sekta ya utengenezaji wa hali ya juu viwandani, ili kuweka msingi imara wa kuhimiza maendeleo ya kisasa ya China.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, alitoa kauli hiyo katika maagizo ya hivi karibuni yaliyowasilishwa kwenye mkutano wa taifa kuhusu sekta ya utengenezaji wa hali ya juu viwandani uliofanyika Beijing siku ya Jumatano na Alhamisi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



