Kampuni ya magari ya China Jetour yatoa uungaji mkono kwa mafundi wenye ulemavu nchini Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2026

Kampuni ya magari ya China Jetour imetoa msaada wake kwa mafundi wenye ulemavu nchini Tanzania kupitia mpango endelevu wa hisani ulioandaaliwa mkoani Arusha.

Mpango huo ulioanzishwa chini ya “Jetour Africa Expedition 2026”, umenunua bidhaa nyingi za sanaa za mikono kutoka Shanga, biashara ya kijamii katika Arusha, inayotoa ajira na fursa za kuhimiza ufundi kwa watu wenye ulemavu kwa kupitia utengenezaji wa bidhaa za sanaa za mikono. Naibu meneja mkuu wa Kampuni ya Jetour International Bw. Yuan Anguo, amesema licha ya kutoa ufadhili, mpango huo unaunga mkono wa utengenezaji wa thamani endelevu huku ukihimiza heshima na uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu, ambayo ni sehemu ya lengo la kampuni hiyo ya kunufaisha jamii.

Meneja mkuu wa kampuni ya Shanga By Elewana, Hazel Gumpo, amesema ununuzi wa bidhaa za Shanga unahimiza shughuli endelevu za kiuchumi, kuwawezesha watu hao kupata kipato kupitia ufundi wao na kushiriki zaidi katika shughuli za uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha