Kundi la Houthi la Yemen ladai kufanya shambulizi dhidi ya Riyadh, na kuonesha kupamba moto kwa mapambano kati yake na Saudi Arabia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2026

Picha iliyonukuliwa kutoka kwenye video Machi 6, 2024 ikimwonesha msemaji wa kijeshi wa kundi la Houthi Bw. Yahaya Sarea, akitoa taarifa mjini Sanaa, Yemen. (Xinhua)

Picha iliyonukuliwa kutoka kwenye video Machi 6, 2024 ikimwonesha msemaji wa kijeshi wa kundi la Houthi Bw. Yahaya Sarea, akitoa taarifa mjini Sanaa, Yemen. (Xinhua)

Kundi la Houthi la Yemen limesema limeanza kufanya mashambulizi makubwa ya kuulenga mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh na mji wa Yanbu, ambao ni kituo kikuu cha viwanda na nishati kwenye pwani ya Bahari ya Sham ya Saudi Arabia, na hii imeonesha kupamba moto kwa mapambano kati ya pande hizo mbili.

Taarifa ya Houthi imetolewa jumamosi baada ya milipuko kusikika mara mbili mjini Riyadh. Moshi ulionekana kufuka karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid kaskazini mashariki mwa Riyadh baada ya tukio la pili, huku baadhi ya usafiri wa ndege za abiria ukicheleweshwa.

Mapema kabla ya hapo serikali ya Saudi Arabia ilitoa tahadhari ya tishio kwa usalama wa anga mjini Riyadh na baadaye kuondoa tahadhari hiyo. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mji mkuu wa Saudi Arabia kutoa tahadhari hiyo tangu mvutano kati ya kundi la Houthi na Saudi Arabia ulipozidi kuwa na wasiwasi hivi karibuni.

Msemaji wa kundi la Houthi Bw. Yahya Sarea, amesema mashambulizi dhidi ya Riyadh yalikuwa ni kujibu mashambulizi makali ya Saudi Arabia ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na kundi la Houthi nchini Yemen. Amesema kundi la Houthi litaendelea na operesheni za kulipiza kisasi chini ya kile alichokiita mkakati wa "hatua kwa hatua" hadi Saudi Arabia kusitisha mashambulizi yake kutoka angani na kuondoa vizuizi vyake dhidi ya Yemen.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha