China na Tanzania zasaini makubaliano ya kupanua hospitali ya moyo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 21, 2026

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Tanzania Bibi Grace Magembe (Mbele, kushoto), akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian, baada ya kusaini makubaliano ya upanuzi wa Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inayosaidiwa na China jijini Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 19, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

China na Tanzania zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa upanuzi wa Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inayosaidiwa na China. Kikundi cha 28 cha madaktari wa China nchini Tanzania pia kimetoa zana na vifaa vya matibabu na dawa kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo, ili kusaidia huduma za afya kote nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Tanzania Bibi Grace Magembe, na Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian, kwenye hafla iliyofanyika JKCI jijini Dar es Salaam.

Mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo, utakaotekelezwa katika eneo la Mloganzila nje kidogo ya Dar es Salaam, unafadhiliwa kwa mitaji iliyotolewa na serikali ya China.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Tanzania Bibi Grace Magembe, akiongea kwenye hafla ya kusainiwa kwa makubaliano ya upanuzi wa Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 19, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian, akitoa hotuba kwenye hafla ya kusainiwa kwa makubaliano ya upanuzi wa Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 19, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha