Rais wa China ajibu barua kutoka kwa vijana wa Marekani

(CRI Online) Septemba 22, 2026

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka kwa wanafunzi vijana wa vyuo vikuu 10 vya Marekani ambao wako nchini China kushiriki kwenye shughuli za mawasiliano kati ya vijana wa China na Marekani.

Rais Xi amesisitiza kuwa vijana wa China na Marekani wako kwenye dunia moja, na wanabeba majukumu ya kizama kwa pamoja. Amewataka kuendelea kushirikiana na vijana wengine wa nchi hizo mbili, kujitahidi kuwa warithi, walinzi na waendelezaji wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Marekani, na kuhimiza kuelewana kwa watu na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha