Uganda yageukia uvumbuzi wa kidijitali na AI ili kuchochea ukuaji wa utalii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2026

KAMPALA - Uganda inaweka uvumbuzi wa kidijitali na AI kuwa vichocheo vya ukuaji wa utalii, Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo amesema hayo Jumapili alipokuwa akiongoza shughuli za maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Utalii Duniani zilizofanyika katika eneo la mashariki la Mbale.

Amesema nguvu ya ushindani ya shughuli za utalii itategemea namna inavyotumia kwa ufanisi teknolojia za kidijitali.

"Mtalii wa leo anataka kutambua mtandaoni mahali pa kwenda kutalii, kulinganisha uzoefu, kuwasiliana na waendeshaji wa shughuli za utalii, kuagiza nafasi, kupitia michakato mbalimbali kwa urahisi na kushiriki uzoefu wake mara moja," Museveni amesema. "Kwa hivyo Uganda lazima ihakikishe kwamba biashara zetu za utalii zinaonekana na zinakuwa na nguvu ya ushindani katika sehemu ya soko la kidijitali."

Rais huyo amesema AI inaweza kuisaidia Uganda katika kunadi mahali pa kutembelewa na watalii, kutoa taarifa kwa watembeleaji, kufanya uendelezaji wa shughuli, ushirikishaji wa wateja, usimamizi wa uhifadhi na kuelewa tabia za watembeleaji.

Tom Butime, waziri wa utalii, wanyamapori na mambo ya kale wa Uganda, amesema AI inawapa wadau wa sekta ya utalii vyombo vipya vya kuelewa masoko, kuyafanya matangazo ya kulenga watu kibinafsi, kuboresha uzoefu wa watembeleaji, kuunga mkono uhifadhi na kuunganisha moja kwa moja mawasiliano ya watalii na wafanyabiashara wa ndani.

Butime amesema ufuatiliaji wa dunia nzima unaopatikana kupitia AI na uvumbuzi wa kidijitali sasa lazima ubadilishwe kuwa idadi ya watalii wanaofika na mapato halisi.

"Lazima tubadilishe mivuto kuwa maulizio; maulizio kuwa kuagiza nafasi; kubadilisha kuweka oda kuwa watalii wanaowasili; na kuwawezesha watalii wanaowasili kukaa kwa muda mrefu zaidi; na kuufanya ukaaji huu wa muda mrefu zaidi kuwa mapato ya juu zaidi ya shughuli za utalii" waziri huyo amesema.

Amesema baadhi ya shughuli za awali za kidijitali, kama vile “Utafiti Nchini Uganda”, zimeonyesha uwezo wa nchi hiyo wa kupata ufuatiliaji dhahiri wa duniani kwa shughuli za utalii za Uganda.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara hiyo, nchi hiyo ilirekodi idadi inayovunja rekodi ya watalii milioni 1.64 wa kimataifa waliofika mwaka 2025, rikodi ambayo imefikia ongezeko la asilimia 19.7 ikilinganishwa na vipindi vya awali vya wakati kama huo.

Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Mambo ya Kale imesema kuwa sekta hiyo inachangia asilimia 5.9 ya Pato la Taifa la Uganda na inaunga mkono moja kwa moja utoaji wa nafasi za ajira zaidi ya 876,000 nchi nzima, kati yake wanawake na vijana wamechukua sehemu kubwa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha