China yazindua njia nne za reli ya mwendo-kasi, ikipanua mtandao wa reli wa nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2026

Treni ya kwanza ya reli ya mwendo-kasi ya Yichang-Xingshan, G6888, ikiondoka kwenye Stesheni ya Reli ya Xingshan katika Wilaya ya Xingshan, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, tarehe 28 Septemba 2026. (Picha na Zou Yuanjing/Xinhua)

BEIJING - China, nchi yenye mtandao mkubwa zaidi wa reli ya mwendo-kasi duniani, jana jumatatu imezindua njia nne kuu za reli ya mwendo-kasi ikiboresha usafiri na mawasiliano katika maeneo mbalimbali.

Njia hizo mpya za reli zinaunganisha Xiong'an katika Mkoa wa Hebei na Shangqiu katika Mkoa wa Henan; Xi'an na Ankang katika Mkoa wa Shaanxi; Yichang na Xingshan katika Mkoa wa Hubei; pamoja na Harbin na Yichun katika Mkoa wa Heilongjiang.

Njia hizo mpya zinazopita maeneo ya kaskazini, kaskazini-magharibi, katikati na kaskazini-mashariki mwa China, zitaleta urahisi kwa usafiri wa wakazi, kuboresha maunganisho ya mawasiliano ya maeneo na kuunga mkono maendeleo ya uchumi.

Treni ya mwendo-kasi, inayopita kwenye reli ya mwendo-kasi ya Xiong'an-Shangqiu, ikipita kwenye daraja kubwa juu ya Mto Manjano, Septemba 28, 2026. (Kampuni ya Kundi la Jinan la Shirika la Reli la China/kupitia Xinhua)

"Mara tu njia ya reli ya sehemu hiyo itakapoanza kufanya kazi, usafiri wa haraka zaidi kutoka Xiong'an hadi Shangqiu utachukua saa 2 na dakika 27 tu," amesema Han Yong, naibu mkurugenzi wa kituo cha usafiri wa abiria cha Kampuni ya Kundi la Beijing la Shirika la Reli la China, akiongeza kuwa njia hiyo itaimarisha zaidi mawasiliano kati ya Eneo Jipya la Xiong'an na masoko makubwa ya kaskazini na katikati mwa China.

Katika eneo la kaskazini-magharibi mwa China, njia ya reli ya Xi'an-Ankang yenye urefu wa kilomita 171 inapita katika Milima ya Qinling, ikishinda changamoto ngumu za kijiolojia, wakati huohuo pia inatilia maanani uhifadhi wa mazingira ya asili. Reli hiyo iliyosanifiwa kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa, treni inaweza kusafiri kati ya stesheni zake mbili za mwishoni kwa dakika 45 tu.

Treni ya kwanza ya reli ya mwendo-kasi ya Yichang-Xingshan, G6888, ikionekana kabla ya kuondoka kwenye Stesheni ya Reli ya Xingshan mkoani Hubei, katikati mwa China, Septemba 28, 2026. (Xinhua/Wang Zichen)

Ujenzi wa sehemu ya njia ya reli ya Yichang-Xingshan katikati mwa China ulikabiliwa pia na changamoto kama hizo, kwani reli hiyo inapita Milima ya Daba kupitia handaki refu lililochimbwa kwa kina la urefu wa kilomita 16.9 na daraja kubwa la juu.

Reli hiyo ya Yichang-Xingshan inaunganisha njia kuu mbili za reli ya mwendo-kasi za China, yaani reli ya mwendo kasi ya Shanghai-Chongqing-Chengdu inayopita kwenye Mto Changjiang na reli ya mwendo-kasi ya Zhengzhou-Chongqing, na italeta msukumo mpya kwa maendeleo katika Ukanda wa Uchumi wa Mto Changjiang, Kampuni ya Kundi la Wuhan la Shirika la Reli la China, ambayo ni mwendeshaji wa reli hiyo imesema.

Reli hizo mpya, ambazo zimefunguliwa muda mfupi kabla ya sikukuu ya taifa, zinatarajiwa pia kuongeza idadi ya watalii kati ya miji mikubwa ya China iliyoko kando za njia hiyo, pamoja na watalii kwenye sehemu zenye vivutio kama vile Bwawa la Magenge Matatu la Yichang na misitu ya kijani ya Yichun.

Picha iliyopigwa Septemba 28, 2026 ikionesha treni ya kwanza ya reli ya mwendo-kasi ya Harbin-Yichun ikiendeshwa mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China. (Picha na Zhang Shu/Xinhua)

Picha iliyopigwa Septemba 28, 2026 ikionesha treni ya kwanza ya reli ya mwendo-kasi ya Harbin-Yichun ikiendeshwa mkoani Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China. (Picha na Zhang Shu/Xinhua)

Kampuni ya Kundi la Shirika la Reli la China imekadiria kuwa safari za abiria milioni 284 hivi zimefanyika na zitafanyika wakati wa kipindi cha Sikukuu ya Mbalamwezi na siku za mapumziko ya Sikukuu ya Taifa kuanzia Septemba 23 hadi Oktoba 8.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha