WHO yaunga mkono juhudi za Kenya kukabiliana na Ebola baada ya kuthibitisha maambukizi ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 07, 2026

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linashirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya kuimarisha hatua za udhibiti baada ya Kenya kuthibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, ambaye alifariki katika hospitali moja jijini Nairobi usiku wa Jumatatu.

Taarifa iliyotolewa na WHO mjini Nairobi inasema serikali ya Kenya inaimarisha mwitikio huku ikifuatilia na kuorodhesha watu waliokaribiana na mtu huyo ili kuimarisha ufuatiliaji. Upimaji katika vituo vya kuingilia vilivyo katika hatari kubwa nchini Kenya,  mawasiliano ya wazi kuhusu hatari, na ushirikishwaji wa jamii ndiyo nguzo kuu ya mwitikio huo, ilisema.

Mkurugenzi wa WHO wa Kanda ya Afrika Bw. Mohamed Janabi, amesema Kenya imeweka hatua muhimu za kudhibiti mlipuko na kwamba kipaumbele kwa sasa ni kuchukua hatua za haraka kubaini maambukizi mengine kabla virusi hivyo havijaenea zaidi.

"Tunaziunga mkono juhudi zinazoendelea kuimarisha mwitikio, na kwa hatua za haraka na zilizoratibiwa, tunaweza kuzuia virusi hivyo kupata nafasi ya kuenea na kuzuia uwezekano wa mlipuko mkubwa zaidi," alisema Janabi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha