Lugha Nyingine
Kenya yaingia kwenye tahadhari ya juu baada ya kuthibitisha maambukizi ya kwanza ya Ebola
Kenya imethibitisha kesi ya kwanza kuambukizwa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo ambaye tayari amefariki dunia, hali ambayo imeifanya serikali ya nchi hiyo kuongeza umakini na tahadhari kutokana na mlipuko unaoendelea kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Waziri wa Afya wa Kenya Bw. Aden Duale amethibitisha kuwa aliyekufa ni raia wa Kenya ambaye alikuwa akiishi nchini DRC kwa miaka saba iliyopita. Alianza kuugua takriban mwezi mmoja uliopita na kupata matibabu katika hospitali kadhaa nchini DRC. Baadaye alisafiri kwa barabara hadi Kampala kabla ya kupanda ndege kuelekea Nairobi, na kuwasili tarehe 3 Oktoba.
Alipokuwa mgonjwa alionyesha dalili za ugonjwa huo na kufanyiwa uchunguzi katika hospitali moja jijini Nairobi, na kuthibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



