Wapatanishi wa AU wahimiza kufuata usimamishaji mapigano na kuendelea na mazungumzo mashariki mwa DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2026

Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na Rais mstaafu wa Ethiopia Sahle-Work Zewde (katikati), wote wakiwa ni wajumbe wa jopo la wapatanishi la Umoja wa Afrika (AU), wakifika kwenye mkutano mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), tarehe 5 Oktoba 2026. (Xinhua)

GOMA, DRC - Jopo la Wapatanishi la Umoja wa Afrika (AU) limetoa wito wa kufuata kwa makini ahadi za kusimamisha mapigano na kuendelea kushiriki katika mchakato wa kidiplomasia wa amani unaoendelea baada ya mazungumzo yaliyofanyika Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)—mji muhimu uliotekwa na kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23).

Taarifa iliyotolewa na AU ilisema kuwa, ujumbe wa jopo hilo ulifanya mashauriano mjini Goma mapema wiki hii na wawakilishi wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya ubinadamu, pamoja na kundi hilo la M23.

Ujumbe huo uliongozwa na Sahle-Work Zewde, Rais mstaafu wa Ethiopia na makamu mwenyekiti wa jopo hilo, na wakiwemo pia Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais mstaafu wa Botswana Mokgweetsi Masisi.

"Amani ya kudumu inahitaji mazungumzo ya kisiasa," jopo hilo limesema, huku likihimiza kuendelea na mawasiliano na kushiriki kwa nia dhati kwenye mchakato wa Doha. Limetoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano kamili na mifumo ya ukaguzi na kuzuia vitendo ambavyo vinaweza kuharibu mchakato wa amani.

Qatar imekuwa mpatanishi wa mazungumzo kati ya serikali ya DRC na kundi hilo la M23 tangu Machi 2025 na kuendesha raundi kadhaa za mazungumzo, hivyo huu mchakato umejulikana kuwa ni mchakato wa amani wa Doha.Mazungumzo hayo hatimaye yalihimiza kusainiwa kwa azimio la kikanuni mwezi Julai 2025 na makubaliano ya kimfumo mwezi Novemba, ambapo pande hizo mbili ziliahidi kujenga hali ya kuaminiana kwa kupitia mazungumzo, kusukuma mbele hali ya utulivu hatua kwa hatua na kushughulikia matatizo ya chanzo cha mgogoro huo.

Jopo hilo pia limesisitiza hitaji la dharura la kulinda raia na kuhakikisha ufikiaji salama na usio na vizuizi wa misaada ya ubinadamu. Limesema kuwa matokeo ya mashauriano hayo yatafikishwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) na serikali ya DRC, wakati huohuo juhudi za kufanya mawasiliano ili kujenga hali ya kuaminiana na kusukuma mbele mchakato wa amani.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Goma jana Jumatano, Corneille Nangaa, kiongozi wa Muungano wa Mto wa Kongo (AFC)—muungano wa kisiasa na kijeshi unaoshirikiana na kundi la M23 ametoa wito wa kuwataka wapatanishi na waratibu "kwenda mbali zaidi ya taarifa za jumla."

Nangaa amesema juhudi za upatanishi zinapaswa kuzaa "ahadi zenye malengo sahihi, za wazi na zinazoweza kuthibitishwa," zikiambatana na mifumo ya kufuatilia utekelezaji wake. Pia amesema kuwa kama mchakato wa Doha utaweza kuendelea, ni lazima kuondoa sababu za chanzo cha mgogoro huo na kuhakikisha hatua halisi za kulinda raia.

Corneille Nangaa (kulia), kiongozi wa Muungano wa Mto Kongo —muungano wa kisiasa na kijeshi unaoshirikiana na kundi la M23 akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Oktoba 7, 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha