Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 yazindua medali na mwenge

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2026

Wafanyakazi wakionesha sare na vifaa kwenye hafla ya kuhesabu siku 100 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 mjini Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, Oktoba 7, 2026. (Xinhua/Xu Chang)

CHANGCHUN - Medali, mwenge, sare na vifaa kwa ajili ya Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 vimezinduliwa jana Jumatano kwenye hafla ya kuhesabu siku 100 kabla ya kufanyika kwa michezo hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonesho ya Anga cha Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China.

Mwenge huo, uliopewa jina la "Ji Xiang" au "Safari ya Heri," umehamasishwa na ua la clivia, ambalo ni ua la mji huo wa Changchun. Sehemu yake ya juu ina mapambo ya utepe wa filamu na alama 12 zinazowakilisha aina za michezo hiyo ya majira ya baridi, ikirejelea tasnia ya filamu ya Changchun.

Medali hizo, zilizopewa jina la "Ji Meng" au "Ndoto ya Heri", upande wake wa mbele una michoro iliyohamasishwa na makali ya viatu vya kuteleza kwenye barafu na njia za kuteleza kwenye theluji, huku upande wa nyuma ukionesha "Ndege wa Kwanza wa Jade wa China ya Kale," kitu cha kale kilichofukuliwa kwenye eneo la kihistoria la Wutaishan huko Nong'an, Changchun.

Chipu ya NFC iliyowekwa ndani ya medali hizo inawawezesha wanamichezo kupata picha zao za hafla za kukabidhiwa medali na mandhari ya misimu yote kutoka Changchun kwa kugusa medali hizo na simu janja.

Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 itafanyika kuanzia tarehe 15 hadi 25 Januari, huku mashindano yakifanyika mjini Changchun na mji wa Jilin ulio karibu.

Leonz Eder, Rais wa FISU, akizungumza kupitia video kwenye hafla ya kuhesabu siku 100 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 mjini Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, tarehe 7 Oktoba 2026. (Xinhua/Xu Chang)

Picha iliyopigwa tarehe 7 Oktoba 2026 ikionesha muundo wa mwenge wa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 ambayo itafanyika mjini Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, tarehe 7 Oktoba 2026. (Xinhua)

Picha iliyopigwa tarehe 7 Oktoba 2026 ikionesha muundo wa medali za Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 ambayo itafanyika mjini Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, tarehe 7 Oktoba 2026. (Xinhua)

Mtumbuizaji akicheza dansi kwenye hafla ya kuhesabu siku 100 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi ya Changchun 2027 mjini Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, tarehe 7 Oktoba 2026. (Xinhua/Xu Chang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha