Majaribio mapya ya chanjo dhidi ya Ebola yaanza nchini Uganda

(CRI Online) Oktoba 09, 2026

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Afrika CDC), kimesema chanjo pendekezwa dhidi ya virusi vya Ebola vya aina ya Bundibugyo imeingia katika kipindi kipya cha majaribio ya kimatibabu nchini Uganda, wakati huu ambapo juhudi zinaendelea kwa kasi kutengeneza chanjo dhidi ya virusi hivyo vinavyochochea mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ofisa wa Afrika CDC Bw. Wessam Mankoula amesema kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika kwa njia ya mtandao jana Alhamisi kuwa kipindi hicho cha pili cha majaribio ya chanjo hiyo (ChAdOx1 BDBV) iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford kilianza Oktoba 6 nchini Uganda kufuatia uzinduzi wa kipindi cha kwanza nchini Uingereza mwezi wa Julai.

Amesema, chanjo nyingine iliyotengenezwa na kampuni ya Moderna imepata idhini ya kimaadili kwa kipindi cha pili cha majaribio nchini Uganda Oktoba 7, baada ya kipindi cha kwanza cha majaribio kuanza nchini Canada mwanzoni mwa Agosti.

Mlipuko huo unaoendelea sasa umesababishwa na virusi vya Ebola vya aina ya Bundibugyo, ambapo hadi sasa hauna chanjo au matibabu yaliyoidhinishwa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha