Shirika la Afrika la kukadiria uwezo wa mkopo (AfCRA), lililopewa mamlaka na AU lazinduliwa rasmi nchini Mauritius

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2026

Picha hii iliyopigwa Oktoba 7, 2026 ikionesha nembo ya Shirika la Afrika la Kukadiria Uwezo wa Mkopo (AfCRA), taasisi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Afrika (AU), mjini Balaclava, Mauritius. (Picha na Ally Soobye/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 7, 2026 ikionesha nembo ya Shirika la Afrika la Kukadiria Uwezo wa Mkopo (AfCRA), taasisi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Afrika (AU), mjini Balaclava, Mauritius. (Picha na Ally Soobye/Xinhua)

PORT LOUIS - Hafla ya uzinduzi wa Shirika la Afrika la Kukadiria Uwezo wa Mkopo (AfCRA), taasisi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Afrika (AU), imefanyika Jumatano wiki hii mjini Balaclava, kaskazini mwa Mauritius.

Shirika hilo la AfCRA lenye makao yake makuu huko Port Louis, mji mkuu wa Mauritius, linalenga kuimarisha namna masoko ya mambo ya fedha ya kimataifa yanavyozifanyia tathmini na kuzielewa nchi zenye mamlaka, mamlaka ndogo za serikali, na kampuni na viwanda vya Afrika, kwa kupitia kukamilisha takwimu, utaalamu na muktadha juu ya hatari ya mikopo barani Afrika, na hivyo kusaidia kuongeza sauti ya Afrika katika usimamizi wa mambo ya fedha duniani.

Shirika hilo ni shirika linalojiendesha kwa kuhimizwa na idara za kibinafsi na kutegemea mitaji inayokusanywa nalo lenyewe, lilianzishwa chini ya usimamizi wa Mfumo wa Uhakiki wa Afrika (APRM) wa AU. AU imesema serikali haziwezi kumiliki hisa kwenye shirika hilo, na hii inalenga kuhakikisha shirika hilo halitapata ushawishi wa kisiasa.

AU imesema ukadiriaji wa mkopo wa shirika la AfCRA utahusisha nchi zenye mamlaka, mamlaka ndogo za serikali, viwanda na kampuni, taasisi za umma na binafsi za Afrika, na linaweza pia kukadiria uwezo wa mkopo wa mashirika nje ya Afrika kutokana na maamuzi ya menejimenti.

Kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Mahmoud Ali Youssouf, alisema kuwa shirika la AfCRA linalenga kuwapa wawekezaji wa Afrika na wa kimataifa, pamoja na washirika wa kiuchumi ripoti zake kuhusu utafiti na uchambuzi wa kuaminika kuhusu uchumi wa Afrika.

Amesema kuwa wakati tathmini za hatari zinapokuwa zikiendeshwa kwa "sababu za kisiasa," gharama kubwa ya mtaji inayotokana na hali hiyo inaweza kuzuia wawekezaji na nchi za Afrika kuwekeza katika miundombinu, afya, elimu, nishati na maendeleo ya viwanda, jambo ambalo litazidisha "shinikizo kubwa la kulipa madeni" linalozikabili nchi wanachama.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na AU, madeni ya Afrika yanayodaiwa nje ya nchi yaliongezeka kutoka dola bilioni 61 za Marekani mwaka 2010 hadi dola bilioni 163 mwaka 2024, huku malipo ya riba yakizidi matumizi ya umma ya sekta ya afya au elimu katika nchi nyingi. Imesema katika hali hiyo, shirika hilo litatafuta namna ya kupunguza mizigo hiyo kwa kupitia kuongeza imani ya wawekezaji na uwazi wa soko.

Takwimu za AU pia zinaonesha kuwa hivi sasa ni nchi 32 tu za Afrika ambazo zimepata ukadiriaji wa uwezo wa mkopo kutoka kwa mashirika makuu matatu ya kimataifa ya kutoa ukadiriaji huo, wakati nchi nyingine zikiwa hazijafanyiwa ukadiriaji. Hivyo, shirika la AfCRA litapanua wigo wake ili kufungua masoko ya mitaji kwa waandaji zaidi wa Afrika. Hata hivyo, Youssouf amesema kuwa shirika la AfCRA halikukusudiwa kuwa mbadala wa mashirika yaliyopo ya kimataifa ya kukadiria uwezo wa mkopo, bali litaungana mkono nayo kwa kutoa "mtazamo wa ziada unaoitilia maanani Afrika."

Wageni wakishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Shirika la Afrika la Kukadiria Uwezo wa Mkopo (AfCRA)—taasisi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Afrika (AU)— mjini Balaclava, Mauritius, Oktoba 7, 2026. (Picha na Ally Soobye/Xinhua)

Wageni wakishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Shirika la Afrika la Kukadiria Uwezo wa Mkopo (AfCRA)—taasisi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Afrika (AU)— mjini Balaclava, Mauritius, Oktoba 7, 2026. (Picha na Ally Soobye/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha