Lugha Nyingine
Je hali inakuaje pale theluji inapoanguka kwa miezi saba katika mwaka?
Kwenye “Mji wa Theluji” (Snow Town) huko Mudanjiang, katika Mkoa wa Heilongjiang kaskazini-mashariki mwa China, theluji huanguka kwa miezi saba kwa mwaka. Hali hiyo inakuaje hasa? Hapo awali, theluji hiyo ilikuwa ni mzigo kwa wenyeji. Ilifunga milima, kuziba barabara, na kufanya shughuli za kazi kusimama kadiri baridi ilivyozidi kuongezeka.
Hata hivyo, kwa sasa ni jambo linalosubiriwa kwa hamu. Nyumba za kulala kwa wageni hujaa kabisa, watu hupanga foleni ili kupata kitoweo kilichopikwa kwenye chungu kikubwa cha chuma, na kauli ya mtalii ya "Wow, pamependeza sana!" inafanya eneo zima kujaa msisimko wa joto—hata wakati halijoto inapokuwa nyuzi joto karibu 20 chini ya sifuri.
Ni theluji hiyohiyo ambayo zamani ilikuwa mzigo kwa maisha ya kila siku, lakini sasa inavutia umati wa watu na kupata umaarufu mtandaoni. Kadiri theluji inavyozidi kuanguka kwa wingi, ndivyo biashara inavyozidi kunoga.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



