Rais wa zamani wa DRC Kabila aongoza muungano mpya wa kisiasa na kijeshi unaojumuisha M23

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2026

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila (katikati) akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

GOMA, DRC - Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila ameteuliwa kuwa kiongozi wa muungano mpya wa kisiasa na kijeshi jana Jumatatu, hatua inayowaweka viongozi wa kisiasa na kijeshi wa kundi la waasi la Vuguvugu la Machi 23 (M23) chini ya uongozi wake.

Muungano huo mpya, unaojulikana kwa jina la Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN), umezinduliwa kwenye hafla iliyohudhuriwa na Kabila pamoja na maafisa waandamizi wa M23 mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini.

Chini ya muundo huo mpya wa uongozi, Corneille Nangaa, kiongozi muhimu katika muungano huo wa waasi, Bertrand Bisimwa, kiongozi mwandamizi wa M23, na Sultani Makenga, kamanda wa kijeshi wa M23, wameteuliwa kuwa makamu watatu wa rais wa FRN.

FRN inakuwa mbadala wa Muungano wa Mto Kongo (Congo River Alliance), muungano wa kisiasa uliokuwa ukishirikiana na waasi wa M23. Pia unaleta pamoja makundi mengine kadhaa yenye silaha.

Tangazo hilo limekuja siku tatu baada ya Kabila, ambaye aliiongoza DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, kutoa hotuba kwa taifa siku ya Ijumaa, akitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo jumuishi ya kitaifa ili kutatua mgogoro wa nchi hiyo.

Tarehe 30 Septemba 2025, Mahakama ya Juu ya Kijeshi ya DRC ilimhukumu Kabila adhabu ya kifo akiwa hayupo mahakamani kwa mashtaka yakiwemo ya uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Kabila alikutwa na hatia ya makosa kadhaa, yakiwemo ya kushiriki katika harakati za uasi, mauaji ya kukusudia, mateso na ubakaji, katika kesi iliyounganishwa na madai ya kuhusika kwake na uasi wa M23 mashariki mwa DRC.

Tangu Januari 2025, hali ya usalama mashariki mwa DRC imezorota kwa kasi, huku kukiwa na mapigano mapya yanayohusisha kundi la M23, ambalo limeteka maeneo kadhaa ya kimkakati, ikiwemo Goma.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila (katikati) akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila (katikati) akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila (katikati) akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila (katikati) akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Mstari wa Mbele kwa ajili ya Kujenga Tena Msingi wa Taifa (Front for the Re-foundation of the Nation-FRN) mjini Goma, makao makuu ya Jimbo la Kivu Kaskazini la DRC, tarehe 12 Oktoba 2026. (Str/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha