Lugha Nyingine
Xi akutana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Togo, na uhusiano wa pande mbili wapandishwa ngazi

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Togo, Faure Essozimna Gnassingbé, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Togo, Faure Essozimna Gnassingbé, mjini Beijing jana Jumanne, ambapo katika mazungumzo yao viongozi hao wawili wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kufikia kiwango cha jumuiya ya China na Togo yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
Xi amesisitiza kuwa urafiki wa jadi kati ya China na Togo ulianzishwa na viongozi wazee wenyewe wa kizazi kilichopita wa nchi zote mbili, msingi wa urafiki huo ni imara na unaimarishwa zaidi kadiri muda unavyopita. Amesema China na Togo zina matarajio ya pamoja juu ya urafiki na ushirikiano, hakika mustakabali utakuwa mpana.
Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kuongeza zaidi ubadilishanaji wa mawazo kwenye ngazi mbalimbali kati ya vyama na nchi hizo mbili, kunufaika pamoja zaidi na uzoefu katika utawala wa nchi, na kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu na mambo yanayofuatiliwa na kila upande.
Xi amedhihirisha kuwa China na Togo zina misimamo sawa juu ya masuala ya kimataifa na kikanda, Xi pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kuongeza uratibu wa mambo ya pande nyingi.
Xi amependekeza kanuni nne zinazolenga kuhimiza pande zote kushiriki kiujenzi katika kutatua matatizo ya mizozo barani Afrika.
Xi amesema, kwanza, ni lazima kushikilia kanuni ya "Afrika kuongoza." Watu wa Afrika ni mabwana kweli wa bara la Afrika na wanapaswa kubeba majukumu yao muhimu katika mambo ya kikanda.
Pili, ni lazima kushikilia usawa na haki. Pande zote zinazoshiriki zinapaswa kufuata nia na kanuni za “Katiba ya Umoja wa Mataifa” na kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.
Tatu, ni lazima kuhimiza usimamishaji vita ili kutimiza amani. Vita na vikwazo vya upande mmoja haviwezi kutatua kimsingi migogoro kati ya nchi. Ni lazima kushikilia kuheshimiana, kufanya mashauriano mapana, kutafuta maoni ya pamoja na kuweka tofauti pembeni, na kufanya zoezi la maelewano na jumuishi.
Nne, ni lazima kushughulikia vyote dalili na vyanzo sababishi. Kazi husika zinapaswa kufuatilia usalama wa hivi sasa pia ni lazima kuweka mipango juu ya maendeleo ya muda mrefu.
Kwa upande wake Faure, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, amesema kuwa katika ziara yake hiyo, ameshuhudia mwenyewe mafanikio makubwa dhahiri ya ujenzi wa mambo ya kisasa nchini China na uendelezaji mpana wa utamaduni bora wa jadi wa China chini ya uongozi wa Rais Xi, na amefahamishwa kwa kina zaidi juu ya wazo la utawala wa China na ufunguo wa mafanikio.
Amesema upande wa Togo unakubaliana kabisa na kanuni muhimu zilizopendekezwa na Rais Xi zinazolenga kuhimiza pande mbalimbali kushiriki kiujenzi katika kutatua matatizo ya mizozo barani Afrika.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Togo, Faure Essozimna Gnassingbé, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



