China na Botswana zaanzisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2026

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakifanya hafla ya kuwakaribisha Rais wa Botswana Duma Gideon Boko na mkewe Kaone Boko kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING – Katika mazungumzo yao mjini Beijing jana Jumanne, Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Botswana Duma Gideon Boko wametangaza kuinua ngazi ya uhusiano wa nchi mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote.

Xi amesema kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na miaka 60 ya uhuru wa Botswana, vyama tawala vya nchi hizo mbili vinapaswa kuimarisha ushirikiano na kuzidisha ubadilishanaji wa mawazo juu ya uzoefu wa utawala wa nchi.

Xi amesema China inaunga mkono Botswana katika kufuata njia ya maendeleo inayolingana na hali halisi ya nchi yao. Ametoa wito kwa pande zote mbili kukamilisha zaidi mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kutumia fursa mpya zinazotokana na sera ya China ya kutoza ushuru-sifuri wa forodha kwa nchi za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China.

“China iko tayari kuimarisha ushirikiano na Botswana katika uchumi wa kidijitali, kilimo, ufugaji na sekta nyinginezo, na kutekeleza mradi wa elimu ya kisasa,” Xi ameongeza.

Kuhusu kuendeleza ushirikiano katika sekta ya madini kati ya China na Botswana na China na Afrika, Xi amesema maliasili za Afrika ni mali ya Afrika, na huo ndiyo msingi wa ushirikiano huo.

Amesema China inapenda kuchangia uzoefu wake na kuzisaidia nchi za Afrika kuandaa mipango ya maendeleo ya madini inayolingana na hali halisi ya nchi zao, na China itahimiza kampuni zake kuhamisha teknolojia za kijani zinazofaa kwa hali ya Afrika.

Xi ameeleza kuwa maliasili za Afrika hazipaswi kuwa vyombo vya ushindani wa siasa za kijiografia, Xi amesema China inakaribisha pande mbalimbali kutoa mchango wa dhati kwa ajili ya maendeleo ya Afrika na China iko tayari kufanya ushirikiano na Afrika, na kujenga mazingira yanayosaidia zaidi uwekezaji na uendeshaji biashara.

Kwa upande wake Boko amesema kuwa China imewasaidia watu wake wenye umaskini kuondokana na umaskini na kufuata njia ya kujiendeleza kwa mafanikio yenye umaalum wa China, ambayo kwayo Botswana ina mengi ya kujifunza.

Amesema Botswana inathamini sana uhusiano wake na China, na itafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kupinga vitendo vyovyote vya kuifanya "Taiwan Kujitenga" na uingiliaji wowote wa nje kwa mambo ya ndani ya China.

“Botswana inapenda kuimarisha hali ya kuhusisha mkakati wa maendeleo na China na inakaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza na kufanya biashara nchini Botswana.” amesema.

Katika ziara hiyo ya kiserikali ya Boko nchini China, nchi mbili zimetoa taarifa ya pamoja juu ya kuanzisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Botswana.

Kabla ya mazungumzo, Xi na mkewe Peng Liyuan walifanya hafla ya kuwakaribisha Boko na mkewe Kaone Boko kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Xi na Peng pia walifanya dhifa ya kuwakaribisha jioni.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Botswana Duma Gideon Boko, ambaye yuko katika ziara ya kitaifa nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Botswana Duma Gideon Boko kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Botswana Duma Gideon Boko kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Botswana Duma Gideon Boko kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Botswana Duma Gideon Boko kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha