Onesho la Opera ya Wu ya China nchini Zimbabwe lawa daraja la kitamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2026

Msanii akitumbuiza jukwaani kwenye onesho la "Opera ya Wu barani Afrika" jijini Harare, Zimbabwe, tarehe 12 Oktoba 2026. (Xinhua/Tafara Mugwara)

Msanii akitumbuiza jukwaani kwenye onesho la "Opera ya Wu barani Afrika" jijini Harare, Zimbabwe, tarehe 12 Oktoba 2026. (Xinhua/Tafara Mugwara)

HARARE - Wasanii wa Opera ya Wu waliovalia mavazi ya kuvutia wamehuisha mila za kale za opera ya China jijini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, Jumatatu wiki hii, wakivutia hadhira kwa ishara zenye hisia, sauti za kuvutia na sanaa ya wushu.

Onesho hilo lilishirikisha tamthilia mashuhuri za Opera ya Wu, zikiwemo "The Goddess of Heaven Scatters Flowers" iliyojaa ustadi na umaridadi, “The Sedan Ride” yenye ucheshi na hisia, na “Three Fights Against the White Bone Demon” iliyojaa vitendo na kusisimua — simulizi pendwa kutoka katika kazi bora ya fasihi ya kale ya China iitwayo “Journey to the West.”

Opera hiyo ya Wu, inayojulikana pia kwa jina la Opera ya Jinhua, yenye chimbuko lake katika Mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China, ni sanaa ya maonesho ya jadi ya jukwaani inayounganisha kwa ustadi uimbaji, sarakasi, na miondoko ya kimitindo ili kusimulia hadithi zisizopitwa na wakati zenye mizizi katika historia na ngano za China.

Zaidi ya mavazi yake ya kuvutia na minyumbuliko migumu ya miili, aina hii ya sanaa inawasilisha mada za kibinadamu za ulimwengu mzima kama vile mapenzi, ujasiri, haki, na kujitolea, ikiwapa watazamaji wenyeji fursa ya kipekee ya kuona utajiri wa utamaduni wa China.

Onyesho hilo la "Opera ya Wu barani Afrika," lililoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Opera ya Wu cha Zhejiang, liliandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa China nchini Zimbabwe, Idara ya Utamaduni, Redio, Televisheni na Utalii ya Mkoa wa Zhejiang, na serikali ya mji wa Jinhua.

Onyesho hilo ni sehemu ya mfululizo wa shughuli za kitamaduni zinazofanyika kote Zimbabwe mwaka huu kusherehekea Mwaka wa Mabadilishano ya Kati ya Watu wa China na Afrika, ambao umepitishwa ili kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na kukuza kuelewana kati ya pande hizo mbili.

Tang Xiaoping, Waziri Mshauri ambaye pia ni Kaimu Balozi wa Ubalozi wa China nchini Zimbabwe, amelielezea onesho hilo kuwa lenye umuhimu katika ubadilishanaji wa pande mbili.

"Kupitia mabadilishano ya karibu zaidi ya kati ya watu na ya kitamaduni, tunaweza kuzidisha kuelewana, kujenga maelewano zaidi, na kuingiza msukumo mpya katika amani na maendeleo ya dunia," alisema Tang.

Tsitsi Gezi, Naibu Spika wa Bunge la Zimbabwe, ameunga mkono kauli hiyo ya Tang. "Onesho linaweza kuwasilisha mambo ambayo wakati mwingine maneno hayawezi, na hivyo kuwezesha uhusiano wa kina zaidi kati ya watu wetu," alisema Gezi.

"Ingawa serikali zinaweza kuweka uhusiano rasmi, ni shughuli kama hizi ndiyo zinazofanya urafiki kuwa wa kibinafsi na wa kudumu." Amesema.

Wasanii wakitumbuiza jukwaani kwenye onesho la "Opera ya Wu barani Afrika" jijini Harare, Zimbabwe, tarehe 12 Oktoba 2026. (Xinhua/Tafara Mugwara)

Wasanii wakitumbuiza jukwaani kwenye onesho la "Opera ya Wu barani Afrika" jijini Harare, Zimbabwe, tarehe 12 Oktoba 2026. (Xinhua/Tafara Mugwara)

Msanii akitumbuiza sanaa ya jadi ya vikaragosi ya Kichina jukwaani kwenye onesho la "Opera ya Wu barani Afrika" jijini Harare, Zimbabwe, tarehe 12 Oktoba 2026. (Xinhua/Tafara Mugwara)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha