Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ataka maendeleo makubwa katika mpango wa "maendeleo ya afya ya China"
Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa juhudi za kufuata kikamilifu njia yenye umaalum wa kipekee za China katika kuendeleza programu za afya, ili kupata maendeleo makubwa katika Mpango wa "maendeleo ya afya wa China " wakati wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, amesema hayo kwenye mkutano wa taifa kuhusu afya uliofanyika Jumatatu na Jumanne mjini Beijing, na kusisitiza kuwa afya ya umma ni kigezo muhimu cha ustawi na nguvu ya taifa.
Tangu mkutano mkuu wa 18 wa taifa a CPC ulipofanyika mwaka 2012, Chama hicho kimefanya uamuzi muhimu wa kuanzisha Mpango wa "maendeleo ya afya wa China," kuhimiza uanzishwaji wa mifumo mikubwa zaidi duniani wa huduma za matibabu, tiba za jadi, kinga na udhibiti wa magonjwa, pamoja na usalama wa afya.
Rais Xi pia amesema China imepata mafanikio ya kihistoria na maendeleo ya pande zote katika sekta ya afya. Hadi kufikia mwaka 2025, wastani wa umri wa kuishi nchini China ulipanda hadi miaka 79.25, huku viashiria vikuu vya afya vikiwa katika nafasi ya juu miongoni mwa nchi zenye mapato ya kati ya juu na nchi zenye idadi ya watu inayozidi milioni 100.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



