Lugha Nyingine
Filamu ya Makala “Safari ya Tembo” yaonyeshwa kwa mara ya kwanza mjini Beijing
![]() |
| Tarehe 21 Oktoba 2026, wageni wakishiriki kwenye sherehe ya kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kwa filamu hiyo mjini Beijing. (Xinhua/Jin Liangkui) |
Filamu ya Makala ya “Safari ya Tembo” (“The Elephant Odyssey”) inasimulia safari ya kiajabu ya kundi la tembo wa Asia waliorandaranda kwenye Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, na safari yao ilivutia watazamaji kote duniani. Filamu hiyo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mjini Beijing jana Jumatano.
Mnamo Machi 2020, kundi hili la tembo liliondoka katika hifadhi ya msitu wa asili iliyopo katika Eneo la Xishuangbanna linalojiendesha la Kabila la Wadai mkoani Yunnan, na kutembea kwa miguu kuelekea kaskazini kwa kilomita 500 hadi kufikia Kunming, mji mkuu wa mkoa huo, mnamo mwezi Juni 2021. Baadaye, walielekea kusini na kurudi kwa usalama katika hifadhi hiyo.
Filamu hii ilitengenezwa kwa ushirikiano kati ya kampuni za filamu za China, Canada na Singapore, na ni jaribio lenye thamani kubwa la kusimulia ulinzi wa ikolojia nchini China.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
