Idadi ya swala wa koo nene yaongezeka wakati mazingira ya ikolojia yakiboreshwa katika hifadhi za mazingira ya asili za Ningxia (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2026
Idadi ya swala wa koo nene yaongezeka wakati mazingira ya ikolojia yakiboreshwa katika hifadhi za mazingira ya asili za Ningxia
Picha iliyopigwa tarehe 17 Oktoba 2026 inaonyesha swala mmoja wa koo nene akionekana kwenye sehemu ya ukingo wa kusini-mashariki mwa Jangwa la Tengger, katika Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya Kitaifa ya Shapotou ya mji wa Zhongwei, Mkoa unaojiendesha wa Ningxia wa Kabila la Wahui, China. (Xinhua/Wang Peng)

Katika miaka ya hivi karibuni, Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya Kitaifa ya Shapotou huko Zhongwei mkoani Ningxia, China imeendelea na kazi za kudhibiti jangwa, na hivyo maeneo ya miti na mimea yameongezeka kwa udhahiri, na sehemu za makazi ya wanyamapori zimeendelea kuboreshwa.

Takwimu za ufuatiliaji zinaonyesha kuwa swala wa koo nene, ambao ni wanyama wa ulinzi wa ngazi ya pili ya kitaifa ya China, wameanzisha makundi kadhaa katika eneo hilo, na idadi yao inaonesha mwelekeo wa kuongezeka kwa utulivu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha