Idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRC yaongezeka na kufikia karibu elfu 10

(CRI Online) Oktoba 27, 2026

Mamlaka za afya na Shirika la Afya Duniani (WHO), zimesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imerekodi wagonjwa karibu elfu 10 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola tangu mlipuko wa ugonjwa huo kutokea mwezi wa Mei, huku mashambulizi makali dhidi ya wafanyakazi wa afya yakileta changamoto zaidi kwa juhudi za kudhibiti mlipuko huo.

Ripoti mpya iliyotolewa jana na mamlaka za afya za nchi hiyo imesema, hadi kufikia Jumamosi iliyopita, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa imefikia 9,964, ikiwemo vifo 4,841, na kiwango cha vifo ni asilimia 48.6.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amelaani shambulizi lililosababisha kifo cha mwuguzi mmoja mkoani Tshopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Bw. Tedros ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii kwamba wafanyakazi wa afya siku zote wanatakiwa kulindwa, huku akitoa mwito kwa usalama na ulinzi wa wale wanaolinda jamii dhidi ya ugonjwa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha