Lugha Nyingine
Bidhaa za kielektroniki na utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu vyachochea ukuaji wa tarakimu mbili katika faida ya viwanda ya China

Picha iliyopigwa Oktoba 19, 2026 ikionesha meli zinazoendelea kujengwa kwenye kituo, Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Wang Chun/Xinhua)
BEIJING – Takwimu rasmi zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) jana Jumanne zinaonesha kuwa ukuaji mkubwa katika tasnia ya elektroniki na utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu vilisaidia kuchochea ongezeko la tarakimu mbili katika faida ya kampuni kubwa za viwanda za China wakati wa miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2026.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, faida za kampuni kubwa za viwanda ziliongezeka kwa asilimia 15.5 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia kipindi kama hicho hadi kufikia yuan trilioni 6.03 (dola karibu bilioni 897.7 za Marekani) wakati wa kipindi cha Januari-Septemba, zikidumisha ukuaji wa tarakimu mbili tangu kuanza kwa mwaka huu.
Zinaonesha kuwa mwezi wa Septemba pekee, faida ya viwanda iliongezeka kwa asilimia 14.4 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa mujibu wa NBS, viwanda vya elektroniki viliibuka kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji, huku faida ikiongezeka mara mbili kutoka mwaka mmoja uliopita na kuchangia pointi za asilimia 9.6 kwenye ongezeko la jumla la faida za viwanda.
Wakati huo huo, takwimu hizo za NBS zinaonesha kuwa faida katika utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu iliongezeka kwa pointi za asilimia 52 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, ikizidi wastani wa jumla wa viwanda kwa asilimia 36.5, kwani mahitaji katika maeneo kama vile nguvu ya mambo ya kompyuta ya AI na miundombinu ya vituo vya data yaliendelea kupanuka.
Takwimu hizo za NBS zinaonesha kuwa katika robo tatu za kwanza, utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu ulichangia asilimia 25.5 ya jumla ya faida inayotokana na kampuni kubwa za viwanda za China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.2 kutoka mwaka uliopita.
Mtakwimu wa NBS Yu Weining amebainisha kuwa kadri utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu unavyoendelea kusonga mbele na nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora zikichukua nafasi kwa kasi zaidi, sekta ya viwanda ya China inabadilika kwa kasi kuelekea muundo wa hali ya juu zaidi na unaoendeshwa na uvumbuzi.
Takwimu za awali zaidi zilionesha kuwa sekta ya viwanda ya China iliendelea kupata kasi katika robo tatu za kwanza za mwaka huu wa 2026, huku pato la viwanda lililoongezwa thamani likiongezeka kwa asilimia 5.3 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.

Picha iliyopigwa Oktoba 27, 2026, ikionesha mitambo na vifaa vinavyosubiri kupakiwa kwenye meli kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi kwenye Bandari ya Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Wang Chun/Xinhua)

Picha iliyopigwa Oktoba 27, 2026, ikionesha mfanyakazi akifanya kazi ndani ya karakana ya kampuni ya nyaya katika Mji wa Gaoyou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Meng Delong/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



