Tanzania yapeleka kampuni na taasisi 36 kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2026

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga waoneshaji bidhaa wa Tanzania wanaokwenda kushiriki kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), jijini Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 31, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Tanzania inapeleka kampuni na taasisi za serikali 36 kushiriki kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yatakayofanyika kuanzia Novemba 5 hadi 10 mjini Shanghai, huku ikitafuta kuongeza mauzo ya nje na kupanua ufikiaji kwenye soko la China.

Ujumbe huo umetambulishwa kwenye hafla ya kuwaaga iliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, ambapo baadhi ya waoneshaji bidhaa washiriki walionesha bidhaa zao, zikiwemo kahawa, chai na asali.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema maonesho hayo yanawapa wafanyabiashara wa Tanzania fursa muhimu kuonesha bidhaa zao, kujenga ushirikiano, na kuvutia wawekezaji kutoka China na masoko mengine ya kimataifa.

Amehimiza washiriki hao kuzungumza kwa hamasa na wanunuzi watarajiwa, kuelewa mahitaji ya soko la China, na kutafuta fursa za kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo pamoja na bidhaa zilizoongezwa thamani.

Mkurugenzi wa Kukuza Biashara katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jonathan Nkwabi, amesema kampuni 36 kutoka sekta ya umma na binafsi zimehamasishwa kushiriki, jambo linaloonesha juhudi za pamoja katika kutangaza bidhaa za Tanzania kimataifa.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, amesema sera ya China ya ushuru-sifuri kwa nchi za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China inafungua fursa mpya kwa wauza bidhaa nje wa Tanzania.

Amesema thamani ya bidhaa zilizoingizwa China kutoka Tanzania ilifikia dola za Marekani milioni 290 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita. Ameongeza kuwa shehena ya kwanza ya asali kutoka Tanzania imeingia kwenye soko la China kupitia njia maalum ya haraka iliyotengwa kwa ajili ya bidhaa za kilimo kutoka Afrika.

Chen amesema aina 15 za bidhaa za kilimo kutoka Tanzania zimepewa idhini ya kuingia kwenye soko la China wakati huohuo kampuni 469 za Tanzania zimejisajili kusafirisha bidhaa za kilimo na chakula kwenda China. Amehimiza wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshiriki kwenye maonesho hayo kutumia jukwaa hilo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na kupeleka bidhaa nyingi zaidi za Tanzania zenye ubora wa juu kwa wanunuzi wa China.

Cathy Wang, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki, amesema kuwa ushiriki wa Tanzania umeongezeka kutoka kampuni sita mwaka 2021 hadi kampuni na taasisi 36 mwaka huu, jambo linaloashiria kuongezeka kwa shauku miongoni mwa wafanyabiashara wa Tanzania kwa soko la China.

Amesema kuwa shirika lake linashirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ili kusaidia waoneshaji bidhaa kukidhi viwango vya uingizaji bidhaa vya China, na kufahamu vema taratibu za uuzaji nje wa bidhaa, uidhinishaji wa forodha, na masuala ya uchukuzi na usambazaji.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian (wa tatu kutoka kushoto), na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dennis Londo (wa pili kutoka kushoto), wakitembelea banda la maonesho lenye bidhaa za mikono kutoka Tanzania, kwenye hafla ya kuwaaga waoneshaji bidhaa wanaokwenda kushiriki kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), jijini Dar es Salaam, Tanzania, tarehe 31 Oktoba, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dennis Londo akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga washiriki wanaokwenda kushiriki kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), jijini Dar es Salaam, Tanzania, tarehe 31 Oktoba, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha