Meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha PLA yawasili Togo kwa ajili ya jukumu la kimatibabu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2026
Meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha PLA yawasili Togo kwa ajili ya jukumu la kimatibabu
Bendi ya Jeshi ikitumbuiza kwa kuipokea meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, Auspicious Ark, mjini Lome, Togo, tarehe 1 Novemba 2026. (Xinhua/Huang Wei)

LOME - Meli ya hospital, Auspicious Ark, ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) imewasili Lome, mji mkuu wa Togo, juzi Jumapili kwa ajili ya ziara ya kirafiki na kutoa huduma za matibabu, ikiwa ni mara ya kwanza kwa meli hiyo ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha China kutembelea Togo.

Katika ziara hiyo, meli hiyo ya hospitali, ambayo inatekeleza jukumu la “Mission Harmony-2026”, itatoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wenyeji ndani ya meli, wakati huohuo timu ya wataalamu wa afya watatembelea hospitali ya jeshi ya Togo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na maarifa.

Ujumbe huo pia utaandaa hafla ya mapokezi kwenye staha ya meli hiyo na mechi ya kirafiki ya mpira wa kikapu dhidi ya wanajeshi wa Togo ili kuimarisha zaidi ubadilishanaji na urafiki.

Tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1972, China na Togo zimedumisha uhusiano mzuri wa pande mbili. Mwezi Septemba 2024, nchi hizo mbili ziliinua uhusiano wao hadi kufikia ngazi ya ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Oktoba 2026, viongozi wakuu wawili wa nchi hizo walitangaza kuinua uhusiano huo wa pande mbili hadi kuwa jumuiya ya China na Togo yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha