Uzoefu wa China wa kudhibiti jangwa wachangia Afrika kujenga "Ukuta Mkuu wa Kijani" (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2026
Uzoefu wa China wa kudhibiti jangwa wachangia Afrika kujenga
Tarehe 20 Septemba 2026, mfanyakazi mmoja akikagua zana ya pampu ya kuchota maji kwa nishati ya jua katika Eneo la Teknolojia ya Kijani la China na Afrika huko Trarza, Mauritania. (Xinhua/Xie Jianfei)

Ingawa kuna umbali wa maelfu ya kilomita kati ya Jangwa la Taklimakan la Xinjiang nchini China na Jangwa la Sahara la Afrika, majangwa hayo mawili yanakabiliwa na changamoto sawa katika kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa.

China ikiwa moja ya nchi zilizoathiriwa vibaya zaidi na hali ya kuenea kwa jangwa, inaendelea kufanya juhudi kubwa za kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa pamoja na kutekeleza miradi mikubwa kadhaa ya kulinda mazingira ya ikolojia, ikiwemo mradi wa ujenzi wa mfumo wa misitu ya ulinzi ya Maeneo Matatu ya Kaskazini mwa China. Kingo za miti ya kulinda mazingira ya ikolojia zenye urefu wa kilomita 3,046 zilizojengwa kwa kuzunguka Jangwa la Taklimakan ni moja ya mafanikio dhahiri ya juhudi hizo.

Katika miaka mingi iliyopita, Xinjiang imefanya utafiti na kufanikiwa kujenga mfumo wenye ufanisi wa kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa, ambao umetambuliwa na nchi za Afrika. Mwaka 2017, Taasisi ya Ikolojia na Jiografia ya Xinjiang ya Taasisi kuu ya Sayansi ya China na shirika la Pan-Afrika la "Ukuta Mkuu wa Kijani" zilitia saini nyaraka za maelewano (MoU) kuhusu kuboresha mazingira ya ikolojia barani Afrika. Uzoefu husika wa China unatumika katika pendekezo la "Ukuta Mkuu wa Kijani" wa Afrika. Pendekezo hilo lililoanzishwa kwa pamoja na nchi 11 za Afrika ikiwemo Mauritania, linalenga kuzuia hali ya kuenea kwa Jangwa la Sahara kuelekea kusini kwa kujenga kingo za misitu zenye urefu wa zaidi ya kilomita 7,000 na upana wa kilomita 15.

Kutoka Taklimakan hadi Sahara, China na Afrika zina matarajio ya pamoja ya kujenga siku za baadaye za kijani zaidi. Ushirikiano wa pande mbili katika kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa unasaidia kubadilisha majangwa makubwa kuwa mandhari ya kijani ya kupendeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha