Bandari ya Yantai, China, yaanzisha mfumo vumbuzi wa kuendesha usafirishaji wa magari nje wenye mambo "manne katika mfumo mmoja" (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2026
Bandari ya Yantai, China, yaanzisha mfumo vumbuzi wa kuendesha usafirishaji wa magari nje wenye mambo
Maofisa wa polisi kutoka kituo cha ukaguzi wa mpaka cha Yantai wakifanya doria karibu na meli ya kubeba magari (ro-ro) ya "SAIC Anji Sincerity" kwenye Bandari ya Yantai mkoani Shandong, mashariki mwa China, Novemba 10, 2026. (Xinhua/Li Ziheng)

Bandari ya Yantai katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, ni bandari muhimu ya pwani kwa biashara ya nje ya magari nchini China, imeanzisha mfumo vumbuzi wa kuendesha usafirishaji wa magari kwenda nje wenye mambo "manne katika mfumo mmoja". Mfumo huu umefungamanisha kazi za magari kuingia au kutoka melini (roll-on/roll-off), kupakia na kupakua makontena ya kawaida, makontena bapa, na ubebaji mizigo isiyo ndani ya kontena.

Hadi sasa, bandari hiyo imefungua njia 21 za kusafirisha magari ya biashara na nje, hatua ambayo imeanzisha mawasiliano kati yake na bandari kuu duniani zinazoshughulikia usafirishaji wa magari. Wakati huohuo, bandari hiyo imeanzisha "njia ya kijani" inayohusisha mnyororo mzima wa viwanda, na kuboresha ufanisi hatua kwa hatua katika kupita utaratibu wa forodha.

Katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, bandari hiyo imesafirisha jumla ya magari 723,000 kupitia njia mbalimbali za usafirishaji, na kufikia ongezeko la asilimia 8.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha