Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China ahutubia hafla ya kufunguliwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la Ushauri wa Biashara la APEC
SHENZHEN - Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, alihudhuria na kutoa hotuba kwenye hafla ya kufunguliwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la Ushauri wa Biashara la APEC siku ya Jumamosi mjini Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.
He, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alieleza kuwa Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa APEC utafanyika hivi karibuni mjini Shenzhen, mkutano ambao utaonesha mwelekeo na kukusanya nguvu kwa ajili ya ushirikiano katika eneo la Asia-Pasifiki.
Ameelezea matumaini yake kuwa Baraza la Ushauri wa Biashara la APEC litaendelea kutukuza na kuhamasisha ujasiriamali wa kuanzisha mambo mapya, kufungua mlango na kufanya uvumbuzi, kuanzisha hali mpya kwa ajili ya APEC kuelekea ujenzi wa jumuiya ya Asia-Pasifiki, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya uratibu na ushirikiano, maendeleo yanayotegemea uvumbuzi, na muunganisho katika eneo la Asia-Pasifiki.
Wakati akihudhuria mkutano huo, He pia alikutana na baadhi ya wawakilishi wa Baraza la Ushauri wa Biashara la APEC na kubadilishana nao maoni juu ya masuala ya kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara katika eneo la Asia-Pasifiki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




