China yarusha chombo cha Shenzhou-24 kwenda kituo cha anga ya juu cha Tiangong kikibeba pia mwanaanga wa kwanza wa kigeni (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2026
China yarusha chombo cha Shenzhou-24 kwenda kituo cha anga ya juu cha Tiangong kikibeba pia mwanaanga wa kwanza wa kigeni
Chombo cha kubeba wanaanga cha Shenzhou-24 kikibebwa kwenye roketi ya uchukuzi ya Long March-2F, kimerushwa kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kaskazini-magharibi mwa China, Novemba 25, 2026. (Xinhua/Li Zhipeng)

JIUQUAN - China imerusha chombo cha kubeba wanaanga cha Shenzhou-24 leo Jumatano asubuhi, kwa kupeleka wanaanga watatu kwenye kituo chake cha anga ya juu cha Tiangong kilicho kwenye obiti, kati ya wanaanga hao akiwemo mtaalamu wa Pakistan wa kilichobebwa (payload specialist).

Chombo hicho kilichobebwa kwenye roketi ya uchukuzi ya Long March-2F kimerushwa kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kaskazini magharibi mwa China.

Wanaanga walio ndani ya chombo hicho ni kamanda wa jukumu hilo na rubani wa vyombo vya anga ya juu Tang Hongbo, mhandisi wa safari za anga ya juu Wu Yi, na mwanaanga wa Pakistan Muhammad Zeeshan Ali, ambaye ni mwanaanga wa kwanza kabisa wa kigeni kutembelea Tiangong.

Jukumu hilo la Shenzhou-24 ni jukumu la kwanza linalotekelezwa kwa pamoja na wanaanga wa China na wa kigeni katika historia ya chombo cha China cha kubeba wanaanga kwenye safari za anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha