Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | Mvumbuzi wa teknolojia wa China asukuma mbele maendeleo ya AI kupitia roboti zenye maumbo ya kibinadamu zinazolenga kuongeza tija (2)
Wakati wa Wiki ya Viongozi wa Uchumi ya APEC 2026 mjini Shenzhen, roboti saba za AlphaBot zilizokuwa kwenye kituo cha vyombo vya habari zilitoa huduma kwa waandishi wa habari wa China na wa kigeni, zikiendeshwa kwa ufanisi wa kutegemeka kwa siku saba mfululizo, ambapo pia zilifanya huduma za kutoa vinywaji.
Roboti hizo zinatoka Ai² Robotics, ambayo ni kampuni mpya ya teknolojia ya mambo ya roboti iliyoanzishwa na Guo Yandong mwanzoni mwa mwaka 2023 mjini Shenzhen. Guo anaona kuwa roboti zenye umbo la binadamu ni lazima zipangiliwe na kutumika katika mazingira halisi kwa ajili ya kutekeleza majukumu halisi.
Akiwa na lengo hilo akilini mwake, Guo ameijenga kampuni ya Ai² Robotics kuelekea kuunda roboti za AI zinazolenga kuongeza tija. Roboti hizo za AlphaBot kwa sasa zimekuwa zinatumika huko Shenzhen katika viwanja vya ndege, viwandani, usimamizi wa miji, na kukabiliana na dharura. Matarajio ya Guo ya kuona roboti zinakuwa kizazi cha nne cha vyombo mahiri kufuatia kompyuta binafsi, simu za mkononi na magari mahiri yanafikia kwa hatua madhubuti kuwa na muundo halisi.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
