Wanaanga wa Shenzhou-24, akiwemo mwanaanga wa kwanza wa kigeni waingia kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2026
Wanaanga wa Shenzhou-24, akiwemo mwanaanga wa kwanza wa kigeni waingia kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China
Picha hii ya skrini iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Anga ya Juu cha Beijing Novemba 25, 2026, ikionesha wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-23 na Shenzhou-24 wakizungumza. (Xinhua/Jin Liwang)

JIUQUAN – Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-24, wakiwemo wanaanga wa China Tang Hongbo na Wu Yi, na mwanaanga wa Pakistan Muhammad Zeeshan Ali, wameingia ndani ya kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China jana Jumatano.

Mtaalamu wa Pakistan Ali ameweka historia kwa kuwa mwanaanga wa kwanza wa nchi ya kigeni aliyeingia kwenye kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China.

Wanaanga hao watatu wanabebwa kwenye chombo cha anga ya juu cha China cha Shenzhou-24 ambacho kilirushwa saa 2:18 asubuhi (kwa saa za Beijing) jana Jumatatu kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kaskazini-magharibi mwa China.

Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-23 katika obiti walifungua mlango wa kituo hicho cha anga ya juu saa 8:35 mchana na kuwakaribisha wageni hao wapya, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).

Baada ya kuingia ndani ya kituo hicho, wanaanga wa Shenzhou-24 walikutana na wanaanga watatu wa Shenzhou-23, ambao wamekuwa katika obiti kwa miezi takriban sita. Wanaanga wa vikundi hivyo viwili kisha walipiga picha ya mkusanyiko wa mara ya tisa wa wanaanga kwenye anga ya juu katika historia ya safari za anga ya juu ya China. Sasa wataanza raundi mpya ya makabidhiano ya majukumu ndani ya obiti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha