“Kongamano la kimataifa juu ya Utafiti wa Lugha na Tamaduni za Afrika 2026” lililoandaliwa na China na Afrika lafanyika Ethiopia (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2026
“Kongamano la kimataifa juu ya Utafiti wa Lugha na Tamaduni za Afrika 2026” lililoandaliwa na China na Afrika lafanyika Ethiopia
Sehemu ya kampasi ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa. (Picha kwa hisani ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing)

"Kongamano la Kimataifa juu ya Utafiti wa Lugha na Tamaduni za Afrika 2026" limefanyika katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 23 hadi 25, Novemba.

Kongamano hilo lililofanyika chini ya kaulimbiu ya "Kubadilishana na Kufunzana kati ya Ustaarabu wa China na Afrika," limeandaliwa kwa pamoja na Chuo cha Utafiti wa Afrika cha Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) na Chuo cha Elimu na Utafiti wa Lugha cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa (AAU), kwa uungaji mkono kutoka Kampuni ya Huawei tawi la Ethiopia. Kongamano hilo ni moja kati ya shughuli muhimu za "Mwaka wa Mawasiliano ya kati ya Watu wa China na Afrika."

Wataalamu na wasomi kutoka vyuo vikuu na taasisi katika nchi mbalimbali zikiwemo za China, Ethiopia, Nigeria, Kenya, Afrika Kusini, Umoja wa Falme za Kiarabu, Benin, na Uingereza wameshiriki kwenye kongamano hilo.

Hafla ya ufunguzi wa kongamano hilo ilifanyika kwenye Mnara wa Jukwaa wa AAU asubuhi ya tarehe 24, Novemba. Mkuu wa AAU Samuel Kifle, makamu mkuu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya CPC katika BFSU, Zhao Gang, pamoja na mwakilishi kutoka Huawei tawi la Ethiopia walitoa hotuba moja baada ya mwingine. Walieleza mchango muhimu wa shughuli za kubadilishana uzoefu za nyanja za lugha na utamaduni katika kujenga kuelewana kati ya watu wa China na Afrika, kuhimiza mazungumzo na kufunzana kati ya ustaarabu, na kuzidisha ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili.

Katika hotuba kuu, mkuu wa Chuo cha Utafiti wa Afrika cha BFSU Li Hongfeng alitoa wasilisho lenye kichwa cha “Mabadiliko na Maendeleo ya Elimu ya Lugha za Kigeni nchini China tangu Sera ya Mageuzi na Ufunguaji Mlango”. Profesa Zelealem Leyew wa AAU alitoa wasilisho juu ya "Masuala ya Kiisimu katika Afrika ya Sasa yenye Lugha Nyingi: Changamoto na Fursa". Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bayero cha Nigeria, Profesa Aliyu Muazu alizungumzia mada ya “Lugha kama Chachu ya Maendeleo ya Taifa – Mtazamo wa Nigeria”.

Kongamano hilo lilikuwa na majukwaa matatu madogo yakijikita katika ufundishaji wa lugha, tafsiri na elimu ya kuvuka tamaduni; kufunzana kati ya ustaarabu na maingiliano kati ya watu; na mienendo ya lugha, fasihi na uchapishaji. Wasomi walioshiriki walijadiliana kwa kina juu ya masuala mapya yanayoibuka na uzoefu wa kivitendo katika nyanja hizo husika.

Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Selamawit Kassa, na Naibu Mkuu wa Taaluma wa AAU Dk. Jeilu Oumer walihudhuria hafla ya ufungaji.

Wasomi hao wamekubaliana kuwa, kongamano hilo limeanzisha jukwaa la wazi, la kivitendo na la masuala mbalimbali kwa ajili ya mabadilishano ya kitaalamu, ambalo linasaidia kujenga kuelewana kati ya jumuiya za wanataalamu wa China na Afrika katika nyanja kama vile lugha na utamaduni, elimu na mbinu za ufundishaji na utafiti wa kikanda na nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha