Lugha Nyingine
Handaki refu zaidi duniani la Barabara Kuu lililojengwa chini ya maji kwa mashine yenye ngao lapata mafanikio muhimu mashariki mwa China (3)
NANJING – Sehemu ya upande wa kulia ya Handaki la Haitai la Mto Yangtze, handaki refu zaidi duniani la Barabara Kuu lililojengwa chini ya maji kwa mashine yenye ngao, imevuka rasmi chini ya Mto Yangtze jana Alhamisi, na kuwa ya kwanza kati ya pande mbili za handaki hilo kufika ukingo wa kusini wa mto.
Mashine ya kuchimba mahandaki iliyoundwa na China yenyewe kwa kujitegemea imekamilisha kazi ya uchimbaji ya urefu wa kilomita 7.46 chini ya mto.
Mashine hiyo ya kuchimba mahandaki, inayoitwa Jianghai, inaweza kuchimba handaki lenye kipenyo cha hadi mita 16.64. Ilianza kuchimba kutoka ukingo wa kaskazini mwezi Aprili 2025 na kuingia sehemu ya chini ya mto Septemba mwaka huu.
Uvukaji huo ulichukua miezi takriban 14, huku mashine hiyo ikisonga mbele kwa wastani wa mita 20 kwa siku, kwa mujibu wa Meng Defeng, ambaye anasimamia uchimbaji wa kutumia mashine hii yenye kinga maalumu kwa Kampuni ya Idara ya 14 ya Shirika la Reli la China kwenye mradi huo.
Handaki hilo ni hatua muhimu katika kujenga barabara kubwa ya kuvuka mto chini ya Mto Yangtze, mto mrefu zaidi wa China, likiunganisha Haimen katika Mji wa Nantong na Taicang katika Mji wa Suzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China.
Likiwa na urefu wa jumla wa kilomita takriban 39.07, handaki hilo linajumuisha sehemu ya chini ya maji yenye urefu wa kilomita 11.185 inayoundwa na njia mbili sambamba.
Baada ya kufunguliwa, handaki hilo litafupisha safari kutoka Nantong hadi kusini mwa Jiangsu na Shanghai, na kuboresha miunganisho ya barabara katika Delta ya Mto Yangtze.
China ilitoa mpango mwezi Julai mwaka huu wa kuendeleza kwa kina maendeleo yenye sifa bora ya huduma jumuishi za usafiri katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), Wizara ya Uchukuzi ya China ilitangaza. Mpango huo unalenga kwa kiasi kikubwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa huduma ya usafiri jumuishi ifikapo 2030.
Chini ya mpango huo, China itaboresha miunganisho kati ya njia mbalimbali za usafiri, kufanya abiria kubadilisha usafiri kuwa rahisi zaidi na kuboresha huduma za usafirishaji wa mizigo. Pia itahimiza mafungamano kati ya usafiri na utalii, kuboresha huduma katika vituo vya usafiri, na kuimarisha usafiri wa abiria, mizigo na huduma za uwasilishaji mizigo vijijini.

Urejeshaji ikolojia waleta uoto wa kijani kwenye kando za Mto Changjiang huko Wuhan, China

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
