Mji wa Jining, China wajenga kituo cha usafirishaji wa majini kwa kufuata kando ya Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2026
Mji wa Jining, China wajenga kituo cha usafirishaji wa majini kwa kufuata kando ya Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou
Picha iliyopigwa Novemba 26, 2026, ikionesha meli inayotumia nishati mpya ya kubeba kontena ikisafiri kwenye Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou katika sehemu yake ya Jining, mkoani Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei)

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Jining mkoani Shandong, mashariki mwa China, umekuwa ukitumia vizuri eneo lake muhimu la kimkakati kwenye sehemu ya kati ya Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou ili kujiendeleza kuwa kituo cha usafirishaji wa majini kwa kufuata kando za Mfereji Mkuu katika eneo la kaskazini mwa China.

Mpaka hivi sasa, Mji huo umefungua njia 33 za usafirishaji wa makontena za kupita sehemu mbalimbali zilizoko mbali na pwani za bahari pamoja na njia 5 unganishi za ndani ya China kwa ajili ya biashara na nje, zikiunganisha masoko katika maeneo ya Delta ya Mto Changjiang, Shanxi-Shaanxi-Mongolia ya Ndani, na Beijing-Tianjin-Hebei.

Kuanzia Januari hadi Oktoba 2026, bandari za mji huo zilishughulikia usafirishaji wa tani milioni 114 za mizigo, na kiasi cha usafirishaji wa makontena kimefikia TEU 532,000.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha