人民网首页

Maoni ya Kimataifa

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kuongeza uelewano na urafiki: Mabalozi

NEW YORK – Konsela mkuu wa ubalozi wa China katika Mji wa New York nchini Marekani Huang Ping amesema kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 siyo tu itaongeza maelewano na urafiki kati ya nchi na sehemu mbalimbali, lakini pia itaongeza imani na matumaini kwa binadamu kushirikiana katika kukabiliana na changamoto. Katika Makala yake iliyochapishwa wiki hii na Gazeti la Philadelphia Inquirer, Huang amewaalika wanamichezo kutoka Marekani na duniani kote kukusanyika pamoja mjini Beijing, kutimiza ndoto yao ya Olimpiki, kufahamu utamaduni wa China, na kusalia kumbukumbu zisizosahaulika za Olimpiki ya Majira ya Baridi maishani yao.

Iliyopita3 4 5 6 7