人民网首页

Maoni ya Kimataifa

China yathibitisha maafisa wa Marekani kutuma maombi ya viza ya kuhudhuria Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 ukioneshwa kwa umma katika Bustani ya Shougang huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 13, 2021. (Xinhua/Zhang Chenlin) BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amethibitisha kuwa China imepokea maombi ya viza kutoka kwa wafanyakazi husika wa Marekani ya kuhudhuria Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.

“China ina uzoefu wa kutosha wa kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi”

Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 ukioneshwa kwenye ziara ya Maonesho ya Mwenge kwenye Bustani ya Shougang, Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 13, 2021. (Xinhua/Zhang Chenlin) KIEV - Sergey Bubka, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Ukraine (NOC) amesema kwamba China ina uzoefu wa kutosha wa kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022, ambayo itakuwa muhimu katika kukabiliana na changamoto na kuimarisha mshikamano duniani kote.

Mwenge wa Olimpiki wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 ukiwa kwenye Mnara wa Olimpiki wa Beijing. (Xinhua/Wang Yong)

Mwenyekiti Kamati ya IOC asema kuongezeka kwa mivutano ni kinyume na dhamira ya IOC

BERLIN - Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach amesema kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 haipaswi kutumiwa kwa kuongeza hali ya mivutano duniani na kwamba ushiriki wa wanamichezo ni makubaliano ya kimataifa. Bach ameelezea wasiwasi wake kuhusu ushiriki wa wanamichezo baada ya Marekani kutangaza kutotuma maafisa wa serikali kuhudhuria mashindano hayo yatakayofanyika Beijing mapema Mwaka 2022 kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Putin akubali kwa furaha mwaliko wa kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

Kwa mujibu wa ripoti, Msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov hivi karibuni alisema kuwa Rais Vladimir Putin amepokea mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China wa kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 , na baada ya Russia na China kukubaliana katika masuala yote, pande hizo mbili zitatangaza kwa pamoja habari husika. Siku ya Jumatatu ya wiki hii, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alipojibu maswali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa kushiriki matukio makubwa kwa pamoja ni desturi nzuri ya miaka mingi kati ya China na Russia.

Iliyopita3 4 5 6 7 Inayofuata