人民网首页

Habari

Ripoti ya kazi ya serikali ya China: kupinga vikali vitendo vya ufarakanishaji vya “watu wanaotaka kuifanya Taiwan ijitenge na China" na uingiliaji kutoka nje

Ripoti ya kazi ya serikali ya China iliyotolewa tarehe 5 imeeleza kuwa China inapinga kithabiti vitendo vya ufarakanishaji vinavyofanywa na "makundi ya watu wanaotaka kuifanya Taiwan ijitenge na China" na vitendo vya uingiliaji kutoka nje. Ripoti ya kazi ya serikali imesema ni muhimu kuzingatia sera na kanuni kuu za kazi kuhusu suala la Taiwan, kutekeleza mkakati wa jumla wa Chama cha kutatua suala la Taiwan katika zama mpya, kuzingatia sera ya kuwepo kwa China Moja na "Makubaliano ya 1992", na kuhimiza maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya China bara na Taiwan na kutimiza muungano wa taifa.

Mkutano wa Mwaka wa Bunge la Umma la 13 la China wafunguliwa Beijing 

Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) umefunguliwa leo tarehe 5, Machi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. (Xinhua /Ding Haitao) Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) umefunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing hapa Beijing Machi 5, 2022.

Mjumbe wa Bunge la Umma la China anayejikita katika kuendeleza kazi za mikono za China

Hou Zhanying, msanifu wa Sanaa za mikono mwenye uzoefu, ambaye ni Mjumbe wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC), amejitolea kuunganisha umaalumu wa utamaduni wa China katika kazi zake za usanifu wa Sanaa za mkono. Mwaka huu, atawasilisha maoni na mapendekezo kuhusu maendeleo endelevu ya tasnia ya kazi za mikono kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China unaofanyika hapa Beijing, Mji Mkuu wa China.

Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) ukifunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2022. (Xinhua)

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza Mkutano wa Mwaka

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China limeanza mkutano wake wa mwaka mchana wa Ijumaa hii Beijing. Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria ufunguzi wa mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Iliyopita4 5 6 7 8 9 Inayofuata