人民网首页

Habari

Viongozi wa China wajumuika na washauri wa kisiasa kwenye mijadala ya vikundi

Viongozi waandamizi wa China jumapili walijumuika na washauri wa kisiasa wa taifa kwenye mijadala ya vikundi tofauti katika Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC). Viongozi hao wakiwemo pamoja na waziri mkuu wa China Bw.

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping atembelea wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na kushiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Mongolia ya Ndani

Rais Xi Jinping wa China Machi 7 mchana amewatembelea wajumbe kutoka sekta za kilimo, huduma za jamii, na bima za jamii wanaohudhuria kwenye Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China. Pia rais Xi ameshiriki katika majadiliano kwenye kikundi cha wajumbe hao, na kusikiliza maoni na mapendekezo yao.

Ripoti ya Kazi ya Serikali ya China yasisitiza kupambana vikali na uhalifu wa utekaji nyara na usafirishaji haramu wa wanawake na watoto

Ripoti ya kazi ya serikali ya China iliyotolewa tarehe 5 mjini Beijing imeeleza kuwa ni muhimu kupambana vikali na uhalifu wa usafirishaji haramu wa wanawake na watoto, na kulinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya wanawake na watoto. Ripoti ya kazi ya serikali pia imesema ni muhimu kuhakikisha watu wanaishi na kufanya kazi kwa amani na katika mazingira ya kuridhika, na kukuza utulivu wa jamii.

Ripoti ya kazi ya serikali ya China: soko kubwa la wazi litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka duniani kote

Ripoti ya kazi ya serikali ya China kwa mwaka 2022 iliyowasilishwa kwenye mkutano wa bunge la umma tarehe 5, imeeleza kutumia kikamilifu mitaji ya kigeni, na kufungua soko kubwa la China, jambo ambalo hakika litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka nchi zote kujiendeleza nchini China. Ripoti hiyo imeeleza kuwa ni muhimu kupanua maeneo yanayoruhusiwa kuwekezwa na nchi za nje, na kuunga mkono mitaji ya kigeni kuwekezwa katika sera za uzalishaji wa hali ya juu na kati, utafiti na maendeleo, huduma za kisasa, na vile vile katika mikoa ya kati magharibi, na kaskazini mashariki.

Iliyopita3 4 5 6 7 8 Inayofuata