Waandishi wa Habari wakishiriki mkutano wa vyombo vya habari kwa njia ya video kuhusu Mkutabo wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 4, 2022. (Xinhua/Chen Zhonghao) BEIJING - Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China utafunguliwa kesho Jumamosi asubuhi hapa Beijing, msemaji wa Bunge hilo Zhang Yesui amesema leo Ijumaa.
Guo Weimin (wa pili kutoka kulia), Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akijibu maswali kwa njia ya video kutokana na mahitaji ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 wakati wa mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 3, 2022. (Xinhua/Yin Genge) BEIJING - Guo Weimin, Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) Alhamisi wiki hii ameelezea imani kubwa ya China katika hali ya uchumi, akisisitiza umuhimu wa sera ya “maambukizi sifuri ya UVIKO” ya China na kukosoa demokrasia ya Marekani, wakati China inaingia msimu wa mikutano mikuu miwili ya mwaka.
Bw. Feng Bing akieleza kuhusu mji wa kale wa Datong.
Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akizungumza wakati akiongoza mkutano wa kufunga kikao cha 20 cha Kamati ya Kudumu ya 13 ya CPPCC mjini Beijing, Machi 2, 2022. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Kamati ya Kudumu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), chombo cha juu cha maushauriano ya kisiasa cha China, imefunga kikao chake cha 20 cha kamati ya kudumu Jumatano wiki hii hapa Beijing.