Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akihudhuria mkutano wa ufunguzi wa kikao cha 20 cha Kamati ya Kudumu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 1, 2022. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) imekutana Beijing siku ya Jumanne wiki hii kujiandaa kwa mkutano wake wa mwaka wa chombo hicho cha juu cha mashauriano ya kisiasa.
BEIJING - Maofisa Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni wamewasilisha ripoti kuhusu kazi zao kwa Kamati Kuu ya CPC na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC. Viongozi hao waliowasilisha ripoti ni wajumbe wa Ofisi ya Siasa na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na wajumbe wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya China.
Dereva wa basi wa Tianjin Wang Yan ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Tangu aanze majukumu yake Mwaka 2018, Wang ameendelea kuwasilisha maoni na mapendekezo kwa NPC, ambayo yanahusu mawasiliano na huduma za matibabu na afya.
Li Zhanshu,Spika wa Bunge la Umma la China (NPC), akiongoza mkutano wa kwanza wa mashauriano wa Kikao cha 33 cha Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 27, 2022. (Xinhua/Zhang Ling) BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la 13 la Umma la China (NPC), imeanza mkutano wake wa 33 Februari 28 kujiandaa na mkutano ujao wa tano wa mwaka wa Bunge la Umma la 13, utakaofunguliwa Machi 5.