(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.) Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), likiwa ni chombo cha ngazi ya juu cha kutoa ushauri wa kisiasa nchini China, jana Jumatatu lilifanya kikao cha pili katika mkutano wake wa mwaka.
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema, pendekezo alilotoa rais Xi Jinping kuhusu maendeleo ya dunia linalingana na mahitaji ya pande zote, ambalo limeungwa mkono haraka na Umoja wa Mataifa pamoja na nchi karibu mia moja. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi zote katika kutekeleza vizuri pendekezo hilo muhimu, na kutoiacha nyuma nchi yoyote, ili kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Maendeleo ya Pamoja ya Dunia.
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang Jana Jumapili amesisitiza kufanya juhudi za pamoja na kwa hatua madhubuti ili kuhakikisha maendeleo mazuri na endelevu ya kiuchumi na kijamii. Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akishiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha wajumbe wa Mkoa unaojiendesha wa Guangxi kwenye Mkutano wa Tano cha Bunge la Umma la 13 la China mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 6, 2022.
(Picha inatoka CRI.) Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ipasavyo kuboresha uwezo wa uzalishaji wa kilimo, na kuendelea na juhudi za kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya huduma za jamii.