Taarifa rasmi iliyotolewa Jumapili iliyopita ikisema kuwa, wajumbe 2,296 waliochaguliwa watahudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Wajumbe hao walichaguliwa kwa kufuata njia iliyowekwa na Kamati Kuu ya Chama, na kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama na Kamati Kuu ya Chama chini ya mwongozo wa fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.