Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China Jumatano iliyopita zilionyesha kuwa thamani ya biashara ya huduma ya China katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2022 iliongezeka kwa asilimia 20.4 ikilinganishwa na ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Kampuni ya Kundi la Magari ya Jianghuai ya Anhui ilitoa takwimu zikionesha kuwa, thamani ya mauzo ya jumla ya mwezi Septemba limeongezeka kwa asilimia 31.9 ikilinganishwa na ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Wakati wa majira ya mpukutiko, katika Eneo la Fanchang la Mji wa Wuhu wa Mkoa wa Anhui, mashamba mengi ya mpunga yameanza kuvunwa huku wakulima wakivuna mpunga kwa pilikapika wakati hali ya hewa iko nzuri. (Mpiga picha: Zhou Mu/Xinhua).
Ghala la Nafaka Akiba la Taifa la Changle liko kwenye Eneo la Changle, Mji wa Fuzhou, Mkoa wa Fujian, lenye eneo la hekta 18, likiwa ni ghala la nafaka akiba linaloweza kuweka nafaka nyingi zaidi katika Mkoa wa Fujian. Katika miaka ya hivi karibuni, ghala hilo limejenga mfumo wa akili bandia wa kuhifadhi nafaka, kushikilia “kuhifadhi nafaka kwa usalama, kuhifadhi nafaka bila kuchafua mazingira, kuhifadhi nafaka kwa njia za kisayansi”, ambalo limesimamia nafaka kwa pande zote na kwa njia ya kisayansi ili kuhakikisha usalama wa chakula.