Tofauti na wauzaji wa jadi wa matunda katika vijiji vya China, Zhang Xiuxiu alipofanya kazi alijiremba kila mara na kupenda kuvaa nguo za mtindo wa kisasa. Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 33 anaendesha kampuni moja ya biashara ya mtandaoni inayouza matufaha katika Wilaya ya Luochuan, Mji wa Yan’an,ulioko Uwanja wa juu wa Majano, kaskazini magharibi mwa China.
Wateja wakinunua vitu kwenye kituo cha maduka huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong wa Kusini mwa China. (Xinhua/Huang Guobao) Idara ya Takwimu ya kitaifa ya China Jumanne ya wiki hii ilisema, katika mwongo uliopita mapato ya wakazi wa China kimisingi yanaenda sambamba na upanuzi wa uchumi wa nchi, na pengo kati ya mapato ya wakazi wa mijini na wa vijijini limepungua kwa kiasi fulani.
Mkutano wa saba wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika tarehe 9 mjini Beijing, ambapo rais wa China Xi Jinping akiwakilisha Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama ametoa ripoti ya kazi, na kutoa maelezo juu ya rasimu ya ripoti iliyotolewa na Kamati Kuu ya 19 kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Wang Huning ametoa maelezo juu ya rasimu ya marekebisho ya Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Ting Bater akifanya kazi kwenye malisho yake katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China, Septemba 8, 2022.(Xinhua/Liu Lei) Ting Bater ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye alizaliwa mwaka 1955 katika Mji wa Hohhot wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, na kuanza kufanya kazi katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag Mwaka 1974.