Wang Shumao, ambaye ni mwanakijiji wa Mkoa wa Hainan wa Kusini mwa China, alipokuwa na umri wa miaka 18 tayari alikuwa mvuvi mwenye uzoefu, lakini wakati huo hakutegemea atakuwa kiongozi wa kijiji baada ya miaka kadhaa. Wang alizaliwa mwaka 1956 katika Kijiji cha Tanmen cha Mashariki mwa Mkoa wa Hainan.
Balozi na ujumbe wa China katika mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa zimefanya matukio ya kusherehekea mwaka wa 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC), ambapo maafisa na wataalam wa nchi za nje walitoa salamu zao za kuutakia mema Mkutano ujao wa 20 wa Taifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kutazamia ushirikiano zaidi. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Tatiana Valovaya, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani Daren Tang, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Ngozi Okonjo-Iweala na wakuu wengine wa mashirika ya kimataifa na wawakilishi wa kudumu wa nchi mbalimbali mjini Geneva wameeleza kufurahishwa kwao na mafanikio makubwa ambayo China imepata katika muongo mmoja uliopita, na kuutakia mafanikio Mkutano wa 20 wa Taifa wa CPC.
Picha iliyopigwa Mei 22, 2020 ikionyesha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen na sehemu ya juu ya Jumba la mikutano ya umma la Beijing. (Picha: Xinhua) Wajumbe 2,296 watahudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) utakaofanyika hivi karibuni, na wajumbe hao walichaguliwa baada ya kupita mchakato wa kuwachagua kwa makini ipasavyo.
Picha iliyopigwa Mei 22, 2020 ikionyesha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen na sehemu ya juu ya Jumba la mikutano ya umma la Beijing. (Picha: Xinhua) Ofisi husika ya China ilitoa habari zaidi kuhusu kuwachagua wajumbe watakaohudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) baada ya kutangaza Jumapili ya wiki iliyopita kuwa wajumbe wote 2,296 wameshachaguliwa.