人民网首页

Habari

Maafisa Waandamizi wafafanua ripoti muhimu ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ikifanya mkutano na waandishi wa habari Tarehe 24 Oktoba 2022 ili kutambulisha na kufafanua ripoti muhimu ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi punde. (Xinhua/Jin Liangkuai) BEIJING - Ripoti ya Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi punde, ni ilani ya kisiasa na mwongozo wa hatua za kufikia ushindi mpya juu ya ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, afisa mwandamizi amesema Jumatatu.

Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wapitisha marekebisho ya Katiba ya Chama

Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofungwa tarehe 22 hapa Beijing, umepitisha marekebisho ya Katiba ya Chama cha CPC, na kukubali kuyaongeza kwenye Katiba ya Chama, maendeleo mapya ya kinadharia katika Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya tangu Mkutano Mkuu wa 19 wa CPC ufanyike, na kurekebisha na kuboresha maelezo kuhusu malengo ya kufikiwa kwenye Katiba kwa mujibu wa majukumu makuu ya CPC yaliyotajwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20. Pia umebainisha malengo ya kimkakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ya kutimiza mambo ya kisasa ya ujamaa ifikapo mwaka 2035 na kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya ujamaa yenye nguvu ifikapo katikati ya karne hii, yaani kutimiza “Lengo la Pili la Juhudi za Miaka 100”.

Kikao cha kwanza cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 20 ya CPC chafanyika Beijing

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambacho ni chama tawala nchini, imeitisha kikao chake cha kwanza cha wajumbe wote leo Jumapili hapa Beijing. Kikao hicho kimechagua wajumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC, wajumbe wa kamati ya kudumu ya ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC, na katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC.

Gazeti la Umma latoa video ya uenezi ya Chama cha Kikomunisti cha China

Wakati wa kufunguliwa kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Gazeti la Umma linatoa video ya uenezi wa Chama cha Kikomunisti cha China ya “Chama cha Kikomunisti cha China”.

Iliyopita1 2 3 4 5 6 Inayofuata